Walimu wadaiwa kuiba maharage, mahindi ya shule Makambako
Njombe. Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Magegele Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wameitaka halmashauri kuwachukulia hatua za kisheria walimu ambao wamebainika kujihusisha na wizi wa mahindi na maharage ya shule. Wamesema vinginevyo hawatakuwa tayari kutoa tena mchango wa chakula shuleni hapo. Kauli hiyo wameitoa leo Julai 14, 2025…