
Dk Mwinyi ataja mambo matatu atakayoyapa msukumo akipewa ridhaa tena
Unguja. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi, amesema katika kipindi kijacho cha uongozi, atajielekeza kwenye maeneo makuu matatu ambayo yataacha alama isiyofutika atakapomaliza muda wake madarakani. Akitaja vipaumbele hivyo, Dk Mwinyi amesema ni kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kukuza uchumi, na kuboresha huduma za kijamii kwa manufaa ya Wazanzibari wote….