
Othman: Nitaanza na Katiba mpya nikishika dola
Dar es Salaam. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema akipata ridhaa ya kuongoza dola, ataanza na marekebisho ya Katiba ili kuvifanya visiwa hivyo kuwa mikononi mwa Wazanzibari. Othman ameahidi Wazanzibari watakuwa na uhuru wa kuhoji kuhusu mwenendo wa uendeshaji wa Serikali hiyo, kwa sababu Zanzibar ni nchi ya waungwana….