
Lusajo asaka rekodi mpya Tabora United
BAADA ya kushindwa kufanya vizuri Dodoma Jiji na kutua Tabora United mshambuliaji, Reliants Lusajo ametaja sababu iliyomnyima rekodi ya upachikaji mabao msimu uliopita na kuahidi neema msimu huu. Akizungumza na Mwanaspoti, Lusajo alisema hakuwa na msimu mzuri msimu uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara lakini anamshukuru Mungu msimu huu yupo fiti…