
Hiki hapa chanzo cha ahaji ajali migodini
Dar es Salaam. Wakati mara kadhaa Serikali ikinyooshewa kidole pale zinapotokea ajali kwenye migodi, Kamishna Msaidizi Wizara ya Madini, Terrence Ngolo amesema ajali hizo haziwezi kuisha kutokana na watu kukiuka maelekezo ya wataalamu. Amesema wakati mwingine ajali hizo hutokea kwa uzembe hasa pale wachimbaji wanapokiuka maelekezo ya tahadhari yanayotolewa na wataalamu. Ngolo amesema hayo leo…