Kigogo wa NCCR Mageuzi atimkia ACT -Wazalendo
Dar es Salaam. Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Elisante Ngoma ametangaza kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo huku akitaja sababu ni chama chake kupoteza dira katika kupambana na chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM). Ngoma amekuwa miongoni mwa vigogo waliohamia kwenye chama hicho hivi karibuni, akitanguliwa na wakili Peter Madeleka, aliyejitosa ubunge Jimbo la Kivule pamoja…