179 mbaroni Mwanza, yumo anayedaiwa kumuua mwanamke
Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu 179 akiwemo Mkazi wa Nyakasela Kata ya Nyakariro Sengerema mkoani Mwanza, Lupande Ng’wani (43) anayedaiwa kumuua Mwajuma Yugele kwa kumpiga na kitu kizito kichwani. Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 18, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mutafungwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari….