
Kengele ya hatari afya duni kwa bodaboda
Dar es Salaam. Bonny Sagati ni kijana mwendesha bodaboda anayefanya shughuli zake maeneo ya Tegeta mkoani Dar es Salaam. Aghalabu siku yake inaanza mapema mno, kabla hata jogoo hajawika. Akiwa bado na usingizi mzito, anapiga mswaki kwa haraka, anakunjua suruali yake iliyochakaa na kuivaa pamoja na jaketi ambalo halijui lini liliona maji! Saa chache baadaye,…