
Dk Mwinyi aahidi kuondoa utitiri wa kodi, kupanua wigo wa mikopo
Pemba. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi amewahakikishia wafanyabiashara ambao hawajapata mkopo unaotolewa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA), watapata endapo akipata ridhaa ya kuiongoza tena Zanzibar. Pia, amesema watapunguza utitiri wa kodi ili waweze kufanya biashara zao kwa tija. Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 24, 2025…