
Hawa, Tamasha la Yanga Day liliwabeba
Leo Septemba 12 ndiyo kilele cha tamasha la saba la Yanga lijulikanalo kama ‘Wiki ya Mwananchi’ litakalofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Katika kila kilele cha Wiki ya Mwananchi, Yanga hucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na timu kutoka nje ya Tanzania na safari hii itakabiliana na Bandari FC ya Kenya. Yanga…