
MAJALIWA: TUTAYAENZI MEMA YOTE YALIYOFANYWA NA NZUNDA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wataendelea kumkumbuka na kuyaenzi mema yote yaliyoyafanywa na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 21, 2024) alipokwenda kuhani msiba wa marehemu Nzunda, nyumbani kwa marehemu Goba, Dar es Salaam. Marehemu Nzunda alifariki Juni 18, mwaka huu…