Balozi Kombo: Diaspora leteni fursa nyumbani, Serikali itawaunga mkono
Dar es Salaam. Serikali imewahimiza Watanzania waishio ughaibuni kwenye mataifa mbalimbali kuchangamkia fursa zilizoko kwenye maeneo yao na kwamba, Serikali itawaunga mkono pale inapohitajika. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo Ijumaa Machi 14, 2025 wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa biashara ya…