Wingi wa kodi watesa wavuvi Ziwa Victoria, waiangukia Serikali
Buchosa. Wavuvi wanaovua samaki aina ya dagaa ndani ya Ziwa Victoria wameiomba Serikali kuwaondolea wingi wa kodi unaoathiri shughuli zao za uvuvi ndani ya ziwa hilo. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa wavuvi wa dagaa, Juma Bupamba kwenye mwalo wa Gembale (Kisiwani) uliopo Kata ya Bulyaheke kuwa wingi wa kodi umekuwa mwiba kwenye shughuli zao…