KONA YA MSTAAFU: Mei mosi iwakumbuke na wastaafu waliokuwa wafanyakazi
Wiki saba zijazo nchi yetu itajiunga na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi (Mei mosi), tunayoaminishwa kuwa, ni kwa ajili ya wafanyakazi na sio wastaafu, ambao labda watakuja tengewa siku yao, japo kitaifa tu! Maana tunaaminishwa pia, ukisha achia ngazi mchuma uondoke, wewe ni mstaafu na Siku ya Wafanyakazi haikuhusu tena, japo ulikuwa ni mfanyakazi,…