Ndoa ya ‘majuu ilivyomtesa Aziz
Aziz ni kijana wa miaka 24 wa Kipalestina aliyekimbia udhalilishaji kwao akaishia kudhalilika majuu. Kisa hiki kinafikirisha, kusikitisha na kufundisha. Wapo wengi kama Aziz walioharibikiwa baada ya kuolewa wakidhani wameoa majuu. Aziz, akiwa hajui hata Kiingereza, alijikuta akijiingiza kwenye ndoa ya mateso. Nkwazi alimjua Aziz. Alikuwa rafiki wa kaka yake aliyemlalamikia kuwa mdogo wake alikuwa…