
Serikali yajitosa matibabu aliyekosa Sh200,000 za upasuaji
Mbeya. Siku moja baada ya Mwananchi kuchapisha habari kuhusu Pascolina Mgala (20), mwenye uvimbe mguuni aliyeteseka kwa miaka tisa akiwa ndani, Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, imejitokeza kusaidia matibabu yake. Pia wadau mbalimbali kupitia makundi ya WhatsApp ndani ya Mkoa wa Songwe, wameguswa na hali ya Pascolina na kuanzisha…