
SHULE MPYA YA MAPINDUZI KUWAONDOLEA ADHA YA UMBALI WANAFUNZI
Na Mwandishi Wetu, Handeni HALMASHAURI ya Mji Handeni mkoani Tanga imeandika historia mpya baada ya kukamilisha ujenzi wa Shule ya Amali ya Mapinduzi, hatua itakayowaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali wa kilometa 22 kila siku kufuata elimu katika Shule ya Sekondari Kwenjugo. Mradi huo uliofadhiliwa na serikali kupitia Mpango wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP)…