
Malipo ya kidijitali, urahisi unaotaka umakini kimatumizi
Iwe unanunua katika duka la rejareja au unaagiza chakula mtandaoni, kulipa si changamoto tena kwani salio hupunguzwa moja kwa moja. Hakuna tena foleni ndefu wala usumbufu wa kutafuta chenji; kila kitu hukamilika kwa sekunde chache tu. Urahisi huu wa mifumo ya kielektroniki umekubalika kwa kasi miongoni mwa Watanzania, ukirahisisha biashara na kupunguza kabisa hitaji la…