
Haya ndiyo machungu wanayopitia wanawake maishani
Acha niwape ‘story’ ya yanayomsibu mwanamke. Ninapogombana na mwanaume, anaponipiga makofi, kunikata na visu, kunipiga na mabapa ya panga hata kunitishia kunichoma na bisibisi, dunia nzima itanishikia kiuno. Wengi wakiwamo wanawake wenzangu watanyanyua midomo yao juu kama chuchunge bila kujua ninachopitia na mahakimu wasiosomea watatoa hukumu zao kwamba mimi ndio tatizo na kwa yaliyonikuta ni…