
ZEC yabaini jambo fomu za urais za Othman, ACT- Wazalendo yatoa msimamo
Unguja. Mtiania ya urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, amepewa muda hadi kesho, saa 3:00 asubuhi kukamilisha ujazaji wa fomu za kuomba uteuzi, baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro. Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetoa muda huo wa nyongeza kwa mujibu wa taratibu, ili kumpa fursa mtiania huyo kurekebisha dosari zilizobainika….