
Sababu Lissu kuomba muda zaidi, Mahakama yatoa kauli
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu ameiomba Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, impe muda apitie uamuzi wa kesi zilizowasilishwa na upande wa mashtaka walipojibu hoja za pingamizi lake alizowasilisha katika kesi ya jinai inayomkabili. Katika kesi hiyo, Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume cha kifungu…