Simba Washikwa Shati na Mtibwa Sugar

Dakika 90 za mchezo wa kukatana shoka kati ya Simba SC na Mtibwa Sugar zimekamilika kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, huku timu hizo zikigawana pointi baada ya sare ya bao 1–1.Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mpanzu aliyefunga katika dakika ya 18, na kuwapa wekundu hao uongozi wa mapema. Hata hivyo, Mtibwa…

Read More

Kipa wa Taifa Stars Hussein Masalanga Atua Yanga

Klabu Yanga leo Jumapili, Januari 18, 2026 imetangaza kukamilisha usajili wa kipa Hussein Masalanga akitokea klabu ya Singida Black Stars. Masalanga aliisaidia Taifa Stars kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza na kuandika historia ya kuwa golikipa wa kwanza kucheza hatua ya 16 bora ya michuano…

Read More

Kihongosi asisitiza umoja, mshikamano na upendo

Manyoni. Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kenan Kihongosi amewataka viongozi na wananchi kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na upendo. Kihongosi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 18,2026 wakati wa mapokezi katika ofisi ya CCM Wilaya ya Manyoni ambayo ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano…

Read More

Kufukuliwa mto Delhu kwarejesha tabasamu

Moshi. Wananchi wa maeneo ya Kisangesangeni na Mauru, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameeleza matumaini mapya ya kuondokana na adha ya mafuriko pamoja na upungufu wa maji ya umwagiliaji, kufuatia kuanza kwa kazi ya kufukua na kuongeza kina cha maji katika Mto Delhu na kuurejesha katika mkondo wake wa asili. Kazi hiyo inatekelezwa na wataalamu…

Read More

Jeshi lakosolewa kuingilia uchaguzi Uganda, Bobi Wine agomea matokeo

Kampala, Uganda. Waangalizi wa uchaguzi wamelikosoa vikali Jeshi la Uganda (UPDF) kwa kutoa maelekezo yanayohusu mwenendo wa uchaguzi, wakisema hatua hiyo inakiuka misingi ya uhuru na uwazi wa mchakato wa kidemokrasia. Katika taarifa ya NTV Uganda, wachunguzi hao wamesema walishtushwa na tamko la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliyewaagiza wapigakura…

Read More

Asilimia 74 hawajaripoti kidato cha kwanza Mara

Musoma. Asilimia 26.43 ya wanafunzi wote wa kidato cha kwanza waliotarajiwa kuripoti kwa ajili ya kuanza masomo ya elimu ya sekondari kwa kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za umma mkoani Mara, ndio wamekwisha ripoti shuleni hadi sasa. Pia asilimia 85.07 ya wanafunzi waliotarajiwa kuanza darasa la kwanza katika shule za msingi za umma mkoani…

Read More

Nashon: AFCON imeniongezea kitu | Mwanaspoti

KIUNGO mkabaji wa Pamba Jiji, Kelvin Nashon amesema mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2025 yaliyomalizika jana huko Morocco, yamemwongezea uzoefu na kujiamini, jambo ambalo litamsaidia katika Ligi Kuu Bara. Nashon alikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano hiyo Morocco na kuishia hatua ya 16 bora (mtoano) ambayo waliondolewa na wenyeji Morocco…

Read More

Namungo yamwinda mido Chama la Wana

WAKATI zikibakia takribani wiki mbili kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 30, 2026, mabosi wa Namungo wamefungua mazungumzo rasmi ya kuipata saini ya kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Stand United ‘Chama la Wana’, Shaban Zubery Ada. Nyota huyo aliyeifungia Stand United bao moja katika Ligi ya Championship msimu huu, ni miongoni mwa wachezaji…

Read More

Ceasiaa Queens yaongeza straika kujiokoa

KOCHA wa Ceasiaa Queens, Ezekiel Chobanka amesema sababu kubwa ya timu hiyo kutofanya vizuri mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Wanawake ni kukosa mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga mabao. Ceasiaa ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi mbili pekee baada ya kucheza mechi nane hali ambayo imewalazimu benchi la ufundi kufanya tathmini…

Read More