ACT Wazalendo kuifikisha INEC kortini kudai viti maalumu, yenyewe yawajibu
Dar es Salaam. Wakati Chama cha ACT-Wazalendo kikikusudia kuifikisha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), mahakamani kwa madai ya kukosea ukokotoaji wa kura uliosababisha wakakosa wabunge wa viti maalumu, tume hiyo imesema chama hicho hakikupata kura za kuwapa sifa za kupata wabunge wa viti maalumu. Novemba 7, 2025, kwa mujibu wa masharti ya Ibara…