Mgombea ubunge CCM Ngorongoro aahidi kutetea masilahi ya wananchi
Arusha. Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Ngorongoro, Yanick Ndoinyo ameahidi kusimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo hilo na kuhakikisha kila sauti ya mkazi wa Ngorongoro inafikishwa serikalini bila kupotoshwa. Ndoinyo amesema jukumu kubwa la wananchi wa Ngorongoro ni kuhakikisha CCM inapata kura za kutosha ili aingie madarakani kusaidia kuendeleza kasi ya maendeleo…