Matatani tuhuma kuisababishia TTCL hasara ya Sh1.5 bilioni
Dar es Salaam. Mfanyabiashara na mkazi wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, Grey Chilaza na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kulisababishia hasara ya Sh1.5 bilioni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL ). Mbali na Chilaza, mshtakiwa mwingine ni Alex Ngonyani ambaye ni mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma. Washtakiwa hao…