Familia yaiangukia Serikali kupotea kwa mtoto wao
Mbeya. Zikiwa zimepita siku 12 tangu kutoweka kwa mtoto Frank Aliko (10), familia yake imeiangukia Serikali ikiitaka kufanya uchunguzi wa kiintelenjia kufanikisha kupatikana kwake. Frank (10), mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ikulu iliyopo Kata ya Ilomba, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, inadaiwa ametoweka nyumbani tangu Machi 4, 2026 baada ya kupelekwa…