Taifa Stars v Niger Mechi ya hesabu

KIKOSI cha timu ya taifa, Taifa Stars jioni ya leo kinatarajia kushuka kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar kuikabili Niger ikiwa ni mechi ya hesabu za kuisaka tiketi ya kwenda katika Fainali za Kombe la Dunia 2026. Baada ya kukosa tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki fainali hizo za mwakani kutokana na Morocco kuinasa…

Read More

Wengine watatu warejesha fomu ZEC

Unguja. Watiania watatu wa kiti cha urais wamerejesha fomu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilisha masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria, ikiwamo kupata wadhamini 1,000 kutoka mikoa mitano iliyopo Unguja na Pemba. Idadi hiyo inafanya jumla ya vyama vinne kurejesha fomu za kuomba uteuzi kati ya 17 vilivyochukua fomu hizo vikitanguliwa na Chama…

Read More

Wadau nchi 18 kujadili tathmini utekelezaji mipango ya maendeleo

Mwanza. Washiriki zaidi 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki Kongamano la kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (MEL) litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 10 hadi 13, mwaka huu. Kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki na wadau wa maendeleo kutoka nchi 18, litafunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano…

Read More

Mrufani alivyoepa kitanzi kesi ya mauaji ya bodaboda

Arusha. Mahakama ya Rufaa imemuachia huru, Charles Kidaha, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya dereva wa bodaboda, Frank Joseph. Awali, katika Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kidaha pamoja na Kuzenza Jendesha na Joseph Mtema, walishtakiwa kwa mauaji Frank, yaliyodaiwa kufanyika Aprili 26, 2014. Charles alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi…

Read More

Sh800 milioni kujenga kiwanda cha cocoa Kyela

Mbeya. Wakati Chama Kikuu cha Ushirika (Kyela) kikitarajia kutumia zaidi ya Sh800 milioni kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuchakata cocoa, wakulima wilayani humo wamesema hatua hiyo itafungua fursa za kiuchumi na uhakika wa bei. Pia, wamepongeza sera ya mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan aliyeahidi Serikali kuongeza nguvu katika ujenzi wa…

Read More