Wengine watatu warejesha fomu ZEC

Unguja. Watiania watatu wa kiti cha urais wamerejesha fomu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilisha masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria, ikiwamo kupata wadhamini 1,000 kutoka mikoa mitano iliyopo Unguja na Pemba. Idadi hiyo inafanya jumla ya vyama vinne kurejesha fomu za kuomba uteuzi kati ya 17 vilivyochukua fomu hizo vikitanguliwa na Chama…

Read More

Wadau nchi 18 kujadili tathmini utekelezaji mipango ya maendeleo

Mwanza. Washiriki zaidi 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki Kongamano la kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (MEL) litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 10 hadi 13, mwaka huu. Kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki na wadau wa maendeleo kutoka nchi 18, litafunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano…

Read More

Mrufani alivyoepa kitanzi kesi ya mauaji ya bodaboda

Arusha. Mahakama ya Rufaa imemuachia huru, Charles Kidaha, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya dereva wa bodaboda, Frank Joseph. Awali, katika Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kidaha pamoja na Kuzenza Jendesha na Joseph Mtema, walishtakiwa kwa mauaji Frank, yaliyodaiwa kufanyika Aprili 26, 2014. Charles alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi…

Read More

Sh800 milioni kujenga kiwanda cha cocoa Kyela

Mbeya. Wakati Chama Kikuu cha Ushirika (Kyela) kikitarajia kutumia zaidi ya Sh800 milioni kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuchakata cocoa, wakulima wilayani humo wamesema hatua hiyo itafungua fursa za kiuchumi na uhakika wa bei. Pia, wamepongeza sera ya mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan aliyeahidi Serikali kuongeza nguvu katika ujenzi wa…

Read More

Rais Indonesia awafuta kazi mawaziri watano kutuliza waandamanaji

Jakarta. Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto amefanya mabadiliko katika wizara tano, hatua inayoelezwa inalenga kuwatuliza waandamaji. Taarifa iliyotolewa na kiongozi huyo inasema mabadiliko hayo yamechochewa na wananchi kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kushughulikia masilahi ya waandamanaji wanaoitaka Serikali kuchukua hatua kuhusu matatizo yanayoikabili jamii. Miongoni mwa mawaziri walioondolewa ni Waziri wa Fedha, Sri…

Read More

Shinda Mizunguko ya Bure Kila Siku Kupitia Wild White Whale – Global Publishers

Meridianbet, kinara wa michezo ya kubashiri Tanzania, anakukaribisha kwenye promosheni ya mwezi mzima kupitia mchezo wa kasino mtandaoni wa Wild White Whale. Kuanzia tarehe 01 hadi 31 Septemba, kila mchezaji aliyesajiliwa ana nafasi ya kujizawadia mizunguko 50 ya bure kila siku, kwa kukamilisha mizunguko 100 kwa pesa halisi. Hii si bahati nasibu. Haijalishi kama umeshinda…

Read More

Samia ataka Bahi, Manyoni wajiandae kutumia fursa za SGR

Manyoni. Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Bahi mkoani Dodoma na Manyoni mkoani Singida kujiandaa kunufaika na fursa zitakazoletwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR) itakayopita katika maeneo yao. Samia ametoa wito huo kwa nyakati tofauti alipotembelea majimbo ya Bahi na Manyoni, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano…

Read More

Tanesco kuokoa mabilioni iliyotumia kukodi vitendea kazi

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza kuokoa Sh1.3 bilioni kila mwezi, zilizokuwa zikitumika kukodi vitendea kazi vinavyotumika kwenda kuwahudumia Watanzania katika mwaka wa fedha 2024/25. Kutokana na gharama hiyo, shirika limenunua bajaji 100, magari 100 na pikipiki 284 ambazo tayari zimeanza kugawiwa katika ofisi za mikoa na wilaya za Tanesco kote nchini…

Read More