Mbunge Kabati awarejeshea tabasamu wenye ulemavu 13
Iringa. Furaha na shangwe zimetawala katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada ya watu 13 wenye ulemavu kukabidhiwa viungo bandia vya miguu vilivyogharimiwa na Mbunge wa Kilolo, Ritta Kabati kupitia Taasisi ya Ritta Kabati Trust Fund. Wanufaika hao wamesema kwa muda mrefu walikwamishwa na gharama kubwa za viungo saidizi, hali iliyowafanya waendelee kuishi…