Kikongwe wa miaka 91 asimulia machungu kufiwa na mumewe wa miaka 102
Sengerema. Kikongwe Chem Mayala (91), mkazi wa Kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amesimulia machungu aliyopata kwa kufiwa na mumewe Masasila Kibuta (102), siku 60 baada ya kufunga ndoa, akisema katika kipindi hicho kifupi waliishi kwa upendo na amani. Chem aliolewa na Kibuta baada ya mkewe wa kwanza kufariki dunia na waliishi kinyumba…