
Kinachosubiriwa leo kesi ya Mpina kuenguliwa urais ACT- Wazalendo
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma leo Jumatatu, Septemba 8, 2025 inahitimisha usikilizaji shauri la kuenguliwa kwa mgombea urais aliyeteuliwa na Chama cha ACT-Wazalendo kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29. Awali Mahakama hiyo ilielekeza shauri hilo lisikilizwe kwa njia ya maandishi na mawakili wa pande zote waliwawasilisha…