Aliyeshtakiwa kwa kumuua mama yake wa miaka 83,aachiwa
Arusha. Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Bukoba imemwachia huru Deus Boniphace, baada ya kujiridhisha kuwa ushahidi wa upande wa mashtaka haukutosha kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa ndiye aliyemuua mama yake mzazi, Cricencia Boniphace (83). Deus alikuwa akikabiliwa na shtaka la mauaji yaliyodaiwa kutokea Mei 22, 2024 katika Kijiji cha Kihinda, wilayani Kyerwa, ambapo alidaiwa kumshambulia…