SERIKALI YATANGAZA KIMA KIPYA CHA CHINI CHA MSHAHARA SEKTA BINAFSI KUANZIA JANUARI 2026
SERIKALI imetangaza ongezeko la wastani wa asilimia 33.4 katika Kima cha Chini cha Mshahara kwa sekta binafsi, kutoka Shilingi 275,060/= hadi 358,322/=, hatua inayolenga kuboresha ustawi wa wafanyakazi na kuongeza tija katika uzalishaji. Kima hicho kipya kitaanza kutumika rasmi kuanzia Januari 1, 2026, baada ya kukamilika kwa mchakato wa tathmini na ushauri uliofanywa na Bodi…