
Zitto azindua kampeni akiahidi kurejesha heshima ya Kigoma
Kigoma/Dar. Uwanja wa Mwami Ruyagwa, mjini Kigoma umegeuka bahari ya zambarau, umati uliovaa vazi la rangi hiyo ulipofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe. Zitto, kiongozi mstaafu wa chama hicho amesema leo Septemba 6, 2025 kuwa safari yake ya kisiasa iliyoanza mwaka 2015 na kukwama 2020 sasa itaendelea kwa nguvu…