Mahakama Kuu Yafungua Kikao cha Mwaka, Jaji Kiongozi Asisitiza Uwajibikaji
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Mustepher Mohamed Siyani. Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Mustepher Mohamed Siyani, amewasisitiza Majaji, Mahakimu na Wakurugenzi wa Mahakama ya Tanzania kuhakikisha wanatekeleza mikakati inayowekwa na vikao mbalimbali pamoja na kuwasilisha utekelezaji wake kwa wakati. Dkt. Siyani ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Februari, 2026…