Morocco yafuzu Kombe la Dunia, Stars yabakiza mbili

Morocco imekuwa timu ya kwanza ya Taifa barani Afrika kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 nyumbani dhidi ya Niger jana, Septemba 5, 2025 huku Taifa Stars ikibakiza mechi mbili. Ushindi huo ambao Morocco imeupata katika Uwanja wa Prince Moulay Abdallah jijini Rabat, umeifanya ifikishe pointi 18…

Read More

Zoran amvuta Mavambo Libya | Mwanaspoti

BAADA ya aliyekuwa kiungo wa Simba, Debora Mavambo kuachana na timu hiyo aliyoitumikia kwa msimu mmoja aliyojiunga nayo Julai 6, 2024, kwa sasa mchezaji huyo anakaribia kujiunga na Asswehly ya Libya kwa mkataba wa miaka miwili. Mavambo aliyejiunga na Simba akitokea Mutondo Stars ya Zambia na kufunga bao moja tu katika Ligi Kuu Bara huku…

Read More

Raizin ataka 10 zaidi Bara

MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Raizin Hafidh amesema malengo aliyojiwekea msimu huu katika kikosi hicho ni kufunga zaidi ya mabao 10, huku akidai endapo atatimiza hayo itakuwa ni njia nzuri kwake kuwa na mwendelezo mzuri. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa sehemu ya kuirudisha Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Bara alimaliza Championship akiwa kinara wa upachikaji wa mabao…

Read More

Kipa aliyevunjika taya aanza mazoezi mepesi

KIPA wa Tabora United, Fikirini Bakari amerejea uwanjani baada ya kuwa nje akijiuguza kutokana na kudaiwa kuvunjika taya wakati akikiwasha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga iliyowafunga mabao 4-0 wiki iliyopita katika Uwanja wa  Gymkhana jijini Dar es Salaam. Fikirini alisema daktari alimwambia afanye mazoezi mepesi ya kukimbia na kuepuka kukongana na watu, na…

Read More

Bado Watatu – 20 | Mwanaspoti

ALINIPENDA sana na mimi nilimpenda. Alikuwa mwaminifu kwangu na mimi nilikuwa mwaminifu kwake. Alikuwa akisafiri kwa wiki mbili au tatu na kuniacha. Sikuwa na ushawishi wowote wa mwanaume na niliamini huko alikokwenda na yeye hakushawishika na wasichana.Miongoni mwa marafiki zake Sufiani ambao alikuwa akifika nao pale nyumbani alikuwa jamaa mmoja aliyekuwa akiitwa Shefa. Shefa alikuwa…

Read More

Hekaya za Mlevi: Zishtukieni sera za ndoto 

Dar es Salaam. Mimi sijui nina uraibu gani. Hata akipita mwendawazimu anayeongea peke yake, nitahangaika hadi nisikie kile anachosema. Mara kadhaa nimekuwa nikiwasikiliza paka wanaolalama usiku wa manane, nikawa nasikia kama wanaongea kama watu. Wakati mwingine niliogopa kwa kudhani nagombaniwa miye, maana mmoja alisema “ni wanguuu” mwingine akajibu “mwongooo”.  Kwa kutaka kujua kila kitu, najikuta…

Read More

JIMBONI KWA CHONGOLO NI FULL VIBE WAKIMSURI MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA SULUHU HASSAN

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Makambako  YAANI ni full vibe… ni shangwe tu kwa wananchi wa Makambako!Ndivyo unavyoweza kueleza wakati mamia ya wananchi wakiwa wamejitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan  Katika mkutano huo ambao unafanyika mapema asubuhi ya leo Septemba 6,2025 wakimsubiri mgombea Urais kupitia CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan…

Read More