Wakulima wa korosho Lindi wavuna Sh82 bilioni
Lindi. Wakulima wa zao la korosho mkoani Lindi kupitia chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao tayari wameshapata fedha zao katika minada mitano iliyofanyika. Akizungumza baada ya kumaliza mnada wa sita wa zao hilo leo Jumanne ,Desemba 16,2025 Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao, Hassan Dossa amesema kuwa hadi sasa tani 42,000 zimeuzwa…