Dalali wa Mahakama akamatwa, agizo la Dk Mwigulu halijatekelezwa

Arusha. Zikiwa zimepita siku 17 tangu agizo la Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba la kurejeshwa mali za mfanyabiashara wa Arusha, Josephine Shirima, mali hizo bado hazijarudishwa huku Jeshi la Polisi likimshikilia dalali wa Mahakama anayedaiwa kuhusika katika kuchukuliwa kwa mali hizo. Aidha, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Arusha, Dominic Mollel, aliyekuwa anashikiliwa na polisi kwa…

Read More

Morocco yaibeba Stars, ikiifumua Zambia

LICHA ya kuwa nchi ya kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia za 2026, Morocco jioni hii imeifumua Zambia ikiwa kwao kwa mabao 2-0 na kuilainishia Tanzania kumaliza nafasi ya pili katika Kundi E. Mabao yaliyofungwa kila moja kipindi kimoja katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja la Levy Mwanawasa, jijini Ndola, lilififisha tumaini la wenyeji…

Read More

MWANAFUNZI MUHAS ABUNI KIFAA CHA KUPIMA MANJANO BILA KUCHUKUA DAMU.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv MWANAFUNZI wa Uhandisi Tiba kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wamekuja na ubunifu wa kifaa kinachoitwa BiliMeasure, kinachotumika kupima kiwango cha bilirubini inayosababisha homa ya manjano kwa watoto wachanga bila kuchukua sampuli ya damu. Akizungumza katika Maonesho ya Pili ya Ubunifu ya MUHAS (Innovation Week 2026), yaliyofanyika leo…

Read More

Jamii yatakiwa kuwapokea wafungwa uraiani

Mbeya. Jeshi la Magereza mkoani Mbeya limeiomba jamii kuwapokea vizuri wafungwa wanaomaliza muda wao wa adhabu gerezani kurejea uraiani, ili kuwafundisha kutii sheria na kuondokana na uhalifu. Hayo yamebainishwa leo Jumanne Agosti 26, 2025 kwenye maadhimisho ya miaka 64 ya Jeshi la Magereza baada ya uhuru, na Mkuu wa Gereza la Ruanda jijini Mbeya, Christopher…

Read More

Depu aendeleza moto Ligi Kuu, Nsajigwa hali bado tete

LAURINDO Aurelio ‘Depu’ amempatia kocha Pedro Goncalves kile alichohitaji baada ya kufunga bao pekee wakati Yanga ikiichapa Tanzania Prisons. Depu ambaye alitokea benchi kipindi cha pili akiingia kuchukua nafasi ya Mohamed Damaro, dakika ya 78 alifunga bao hilo kufuatia kipa wa Tanzania Prisons, Mussa Mbissa kushindwa kuokoa mpira wa faulo uliopigwa na Allan Okello. Mechi…

Read More

Wananchi watahamaki kupatwa kwa mwezi Dar

Dar es Salaam. Jana, Jumapili Septemba 7, 2025, Tanzania ilishuhudia tukio adimu la kupatwa kwa mwezi ambalo limeacha simulizi tofauti miongoni mwa wananchi. Wakati baadhi ya makundi yalionekana kujikusanya mitaani kushuhudia kwa mshangao anga likibadilika na mwezi kufunikwa kwa kivuli cha dunia, wengine walihisi hofu kubwa na kujifungia ndani kwa imani kuwa ni ishara ya…

Read More

ORYX GAS YATANGAZA KUDHAMINI CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI YA KUPIKIA KATIKA MAKAMBI YAO

Na Mwandishi Wetu,Dodoma KMAPUNI ya Oryx Gas Tanzania imesema inajivunia kutangaza rasmi udhamini wake wa kambi ya Skauti Tanzania, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuendeleza vijana, kulinda mazingira, na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini sambamba na kutoa mitungi ya gesi 260 makubwa na madogo kwa Chama hicho. Akizungumza leo Septemba…

Read More

Mwalimu aahidi kujenga Kariakoo ndogo Nkasi

Nkasi. Ili kukuza uchumi wa wananchi wanaoishi maeneo ya mipakani na kuimarisha fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kimeahidi kuanzisha soko la biashara la ‘Kariakoo ndogo’ katika Kijiji cha Kirando, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa endapo kitachaguliwa kuunda Serikali Jumatano ya Oktoba…

Read More