Nafasi ya huduma rasmi za kifedha katika Dira 2050

Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia mifumo rasmi ya kifedha ikiwemo huduma za benki ili kuiwezesha Tanzania kutimiza malengo ya kuwa taifa lenye uchumi jumuishi na shindani ifikapo 2050. Hayo yalielezwa jana Septemba 04, 2025 wakati wa kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) likilenga kuangazia fursa na changamoto za sekta hiyo katika utoaji…

Read More

NI NYOMI TU KILA ANAKOKWENDA MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DK.SAMIA SULUHU HASSAN

*Aacha matumaini makubwa kwa wakulima wa zao la parachichi ,Chai wilayani Rungwe  *Mashamba ambayo wawekezaji wameshindwa kuyaendeleza Serikali yaunda timu kufuatilia Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Rungwe KAMPENI za mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suhusu Hassan zimeendelea katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambapo maelfu ya wananchi wamejitokeza kwenye mkutano huo. Akiwa katika…

Read More

Rasmi Fadlu afunuliwa faili la Bajaber

WAKATI mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kumuona Mohammed Bajaber akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mechi za mashindano, kocha wa zamani aliyewahi kumnoa wakati akiwa Polisi Kenya, amempa ‘code’ kocha Fadlu Davids aweze kumfaidi vyema kikosini. Bajaber ni kati ya…

Read More

Messi apewa mmoja Polisi Tanzania

TIMU ya maafande wa Polisi Tanzania, imefikia makubaliano ya kumsajili aliyekuwa winga wa Namungo ‘Wauaji wa Kusini’, Issa Abushehe ‘Messi’ kwa mkataba wa mwaka mmoja kukitumikia kikosi hicho, baada ya pande zote mbili kufikia uamuzi huo. Abushehe ameachana na Namungo aliyojiunga nayo katika dirisha dogo la Januari 2025, ikiwa ni muda mfupi tu tangu nyota…

Read More

Simbu, Gisemo kubeba mioyo ya Watanzania Tokyo

MATUMAINI ya Tanzania kuongeza medali ya tatu katika historia ya mashindano ya dunia ya riadha yapo mikononi mwa wanariadha wawili Aphonce Simbu na Josephat Gisemo watakaoshiriki kuanzia Septemba 13, mwaka huu, jijini Tokyo, Japan. Awali, Tanzania ilitarajia kupeperusha bendera kwa wanariadha wanne, lakini mipango hiyo ikayumba baada ya bingwa wa marathoni wa Wanawake, Magdalena Shauri…

Read More

Straika Majimaji ageukia udiwani | Mwanaspoti

MSHAMBULIAJI wa zamani Majimaji, Stand United, Alliance na Singida United, Six Mwasekaga amegeukia siasa akijitosa kuwania udiwani kupitia chama cha ACT Wazalendo katika Kata ya Mbugani, wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya. Mwasekaga aliliambia Mwanaspoti kwa sasa hachezi mpira wa ushindani na ameona ana nafasi ya kufanya kitu katika jamii kupitia siasa. “Kitu kikubwa kilichonishawishi ni…

Read More

Arusha yalenga kuwa kivutio kikuu cha michezo Afcon 2027

Arusha inajiandaa kujipanga kuwa kitovu cha michezo na utalii kwa kuwaleta pamoja wawekezaji na mashabiki wa kimataifa kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027. Maandalizi ya mashindano hayo hayana kasi tu, bali pia yanatoa fursa ya kudumu kwa Arusha kuendeleza sekta ya michezo ambayo ni hatua muhimu katika kuanzisha jiji hilo kuwa kitovu…

Read More

Bajana atua jeshini na mzuka

BAADA ya kuagana na uongozi na wechezaji wenzake wa Azam FC,  kiungo Sospeter Bajana ametua JKT Tanzania akiwa na mzuka mwingi, akisema yupo tayari kwa ushindani ndani ya kikosi hicho anachoamini kitamrudisha katika ubora aliokuwa nao awali. Bajana amemalizana na Azam baada ya kuitumikia kwa miaka 15 na msimu ujao atakuwa na kazi jeshini kuitumikia…

Read More

JKT Queens yaanza kibabe CECAFA Women

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Wanawake, JKT Queens imeanza kwa kishindo michuano ya CECAFA kwa Wanawake ya kuwania tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa JKU Princess mabao 5-0 kwenye mchezo wa Kindi C. Mechi hiyo imepigwa mchana huu kwenye Uwanja wa Ulinzi Complex  Kenya ambako mashindano hayo yanaendelea kufanyika kuanzia jana hadi…

Read More