Chaumma: Tutafuta njaa, tutarudisha tabasamu la Watanzania

Tanga. Mgombea mwenza wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja, ameahidi kurejesha furaha ya Watanzania baada ya kuingia madarakani. Minja amesema kukosekana kwa furaha kunatokana na ugumu wa maisha waliyonayo Watanzania, ikiwemo kupanda kwa bei ya chakula, kodi, ushuru, ukosefu wa ajira pamoja na njaa. Amesema haiwezekani watu wakune vichwa kuhusu kile watakachokula…

Read More

Wavuvi Igombe wapewa elimu ya mpigakura

Mwanza. Wavuvi wa mwalo wa Igombe, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wamepewa elimu ya mpigakura na kuhamasishwa kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili kuchagua viongozi wanaowataka. Elimu hiyo imetolewa leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mwalo huo unaokadiriwa kuwa na wavuvi zaidi ya 5,000. Mvuvi wa mazao ya samaki, Peter Bukanu, amesema elimu aliyoipata…

Read More

Samia aahidi Pwani kuwa kitovu cha usafirishaji, viwanda

Pwani. Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema akipata ridhaa ya miaka mitano mingine Serikali yake itajenga Bandari ya Bagamoyo na kuifanya Pwani kuwa kitovu cha usafirishaji na viwanda nchini. Samia amesema hayo leo Jumapili Septemba 28, 2025 wakati akihutubia mkutano wa kampeni mkoani Pwani katika Uwanja wa Mkuza wilayani Kibaha….

Read More

AICC KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

Na Mwandishi wetu KITUO cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)kimesema kuwa kinaendelea kuboresha kumbi zake mbalimbali huku kikiwakaribisha wadau wa kimataifa na kitaifa kufanya shughuli zao za mikutano katika kumbi zao kutokana na madhari uwepo wa madhari nzuri. Akizungumza leo Septemba 26,2025 wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya 22 ya wahandisi yanayoendelea…

Read More

Azam yafanya kweli, yazifuata Simba, Yanga

MABAO mawili katika kila kipindi katika pambano la marudiano la Kombe la Shirikisho Afrika lililomalizika jioni hii, yametosha kuivusha Azam FC kwenda raundi ya pili ya michuano ya kimataifa ikizifuata Simba, Yanga, Singida BS na KMKM zilizotangulia mapema. Azam iliifyatua El Merreikh ya Sudan Kusini kwa mabao 2-0 katika mechi  iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam…

Read More