Chaumma yaahidi kurejesha viwanda vya kuchakata chai ndani ya siku 100
Njombe. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameahidi kufufua viwanda viwili vya chai vilivyofungwa katika eneo la Lupembe mkoani Njombe. Amesema chama hicho kitafanya hivyo ndani ya siku 100 endapo kitapatiwa ridhaa na wananchi Oktoba 29, 2025. Mwalimu amesema serikali yake haiwezi kuridhia eneo kama la Njombe linalozalisha…