Mamia wajitokeza maziko ya Jenista, Dk Nchimbi akiongoza
Ruvuma. Mamia ya watu wamejitokeza katika kijiji cha Luanda kilichopo Halmashauri ya Mbinga mkoani Ruvuma, kwa ajili ya kuhitimisha safari ya mwisho ya aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama. Jenista ambaye amekuwa mbunge wa Peramiho kuanzia mwaka 2005, alifariki dunia Alhamisi, Desemba 11, 2025 jijini Dodoma, kwa matatizo ya ugonjwa wa moyo. Katika maziko…