Tahadhari zachukuliwa vifo vya samaki Mto Malagarasi
Dar/Kigoma. Serikali mkoani Kigoma imesema wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji kwa matumizi ya nyumbani kutoka vyanzo vingine salama, huku uchunguzi wa kitaalamu ukiendelea kufanywa kuhusu vifo vya samaki na viumbe wengine vilivyogunduliwa ndani ya Mto Malagarasi. Wananchi ambao wamekuwa wakipata maji kwa matumizi mbalimbali kutokana na chanzo hicho, wameacha kuyatumia kutokana na tahadhari iliyotolewa…