KONGAMANO LA TAWEN MBEYA LIMELETA ELIMU NA FURSA
Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) umeendelea kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuwawezesha wanawake na vijana kupitia kongamano kubwa lililofanyika jijini Mbeya, ambapo elimu na fursa mbalimbali ziliwasilishwa kwa washiriki kutoka sehemu tofauti za mkoa huo. Kongamano hilo lilifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Solomoni Itunda, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa…