Moto wateketeza vibanda 20 Masai Market, Iringa
Iringa. Moto mkubwa umeharibu vibanda takribani 20 vya wafanyabiashara katika soko la Masai Market lililopo mjini Iringa. Tukio hilo limetokea katika eneo la Garden, lililopo mkabala na ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, baada ya kuzuka usiku wa kuamkia leo Machi 16, 2026, na umesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara za utalii…