
Wanaodaiwa kuiibia Benki ya Equity Sh5.7 bilioni, waendelea kusota rumande
Dar es Salaam. Mshtakiwa Jasmine Elphas na wenzake 10, wanaokabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ya Sh5.7bilioni kwa udanganyifu mali ya Benki ya Equity Tanzania Limited, wataendelea kusalia rumande hadi Oktoba 6, 2025 wakati kesi hiyo itakapotajwa. Hatua hiyo, inatokana na upelelezi wa kesi hiyo ya uhujumu uchumi…