WANANCHI WAIPONGEZA TANROADS-MOROGORO KWA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA WILAYANI MALINYI
Baadhi ya wananchi katika Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wameipongeza Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuendelea na kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya barabara na madaraja ambayo imeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali. Wamesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo zimesababisha maji kupita juu ya barabara na…