MAANDAMANO CHADEMA: Polisi Dar yakamata waandishi wawili wa Mwananchi
Dar es Salaam. Polisi jijini Dar es Salaam wamewakamata waandishi wa habari wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa nyakati tofauti wakati wakiripoti maandamano ya amani yaliyoitishwa na Chadema. Hata hivyo, mmoja ameshaachiwa. Mpaka sasa jeshi hilo linamshikilia Lawrence Mnubi ambaye ni mpiga picha jongefu (videographer) wa Mwananchi, aliyekuwa eneo la Msimbazi akitimiza…