
Chaumma yazidi kuchanja mbuga yaingia Kilimanjaro
Kilimanjaro. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu, ameendelea na kampeni zake baada ya kuhitimisha ziara ya siku tatu mkoani Tanga na apiga hodi Kilimanjaro, akilenga kuwashawishi wapigakura milioni 37.6 waliojiandikisha kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Katika uchaguzi huo unaosimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi…