
WAWEKEZAJI WA MIGODI HANDENI WATAKIWA KUZINGATIA USALAMA KUEPUKA AJALI
Na Mwandishi Wetu, Handeni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewataka wawekezaji wa migodi ya madini kuhakikisha wanazingatia kikamilifu kanuni na miongozo ya usalama ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika. Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa dhahabu wa GSB uliopo Kilima Mzinga, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mhe. Nyamwese amesema ni jukumu…